SIFA YA SMART ELIMU
Kuhusu smartelimu
Smart Elimu ni jukwaa la kisasa la kujifunzia masomo kwa njia ya picha jongefu, picha mnato, sauti na maandishi. Jukwaa hili lililozingatia Mtaala wa elimu ya Tanzania lina mfumo uliorahisishwa zaidi ili kumfanya kila mtumiaji afurahie. Smart Elimu inaruhusu kujifunza mtandaoni na nje ya mtandao kupitia kompyuta, “tablet”, simu za mkononi na nje ya mtandao kupitia DVD / CD, na Luninga kupitia vitunza kumbukumbu maalum.
Masomo yote kama yalivyoandaliwa katika Mtaala wa Tanzania na masomo mengine ya ziada yamebadilishwa na kuwa Picha jongefu, Picha Mnato, Sauti, Majaribio ya Kisayansi na “Simulations” ambapo mwanafunzi anaweza kutumia kwa njia sawa na ile ya kufundishwa na mwalimu darasani.
Mbali na kuwapa kipato cha ziada walimu wenye uwezo ambao wamechaguliwa kwa umakini kwa kushindanishwa, Smart Elimu inatambua na kuheshimu kazi nzuri za Waandishi wa vitabu wa Tanzania, pia masomo mengine ya ziada yaliyoandaliwa ili kuchagiza Mtaala wa Masomo ulioandaliwa na Serikali. Lengo letu kuu ni kushughulikia changamoto ya upatikanaji wa elimu halisi na bora kwa kila mtoto wa Kitanzania. Smart Elimu pia imeandaa michezo mbalimbali kwa ajili ya watoto wa Elimu ya Awali na Elimu ya msingi ambayo inapatikana bure kwenye jukwaa letu.
.